Some of Siti's Songs
Uchungu wa Mwana
(The pain of raising a child)
Uchungu - hee - wa mwana -hee ajuae Fatuma mzazi
Kapata taabu mashaka na kazi
Ugonjwa ni suna kufa ni faradhi
Uchungu - hee - wa mwana - hee ajuae Fatuma mzazi
Aaaaa na uzawi na uzawi wa tamatiti na binti Soo
Ni mifahali ya nyati uso nicho
Ah! Walidhani sikipati hiki hicho
Uchungu - hee - wa mwana - hee ajuae Fatuma mzazi
Kupata taabu mashaka ni faradhi
******************************************
The Currency in Zanzibar in the 1920's was the Rupee
******************************
Usiweke tamaa Mbele
( Don't let desire rule)
Hiki thawabu tamaa usiweke mbele
hiki thawabu huwadia kila kale na kale mambo
yalo....huwadia
Maadhi ya upole, mara umekwepukia
wala hayawezi kuwepukia
KIBWAGIZO:
Kwepukia, kwepukia, kwepukia mara hukwepukia
Twende mbele, mara hukwepukia
Kaka kukuingia ukatumaini mema
Kaka hukuingia ukatumaini mema
Kama aha, hukwangalia, ah, ah, ah
Tamaa wee tamaa si kitu chema
Mara huja pinduka, tamaa si kitu chema
Ni kheri kuiepuka mali mengi husoma
Ukiwa huna aaa, aaa pa kuyapata
Akupendendaye daima mwisho wee humwepukia
Tamaa siweke mbele, utumaini kwa kifu
Utumaini kwa kifu.

Culture Music Club Violinist Khamis Shehe
Ela Kafa Ndugu Zangu
(Money is Useless My Friends)
Ela Kafa ndugu zangu Wa shamba hata mjini
Mwenye kazi ya Mungu Maliki wa duniyani
Roho mzipige rungu Cha mtu msitamani
Msitamani……
Msicheze na Hakimu ahukumuye mezani
Bure mtajidhulumu kwa akali kitu duni
Na hayo mwayafahamu Jiti la ncha jichoni
Jiti…
(2)
Wala haifai wakili Aliyesoma landani
Bure atalia mali Upelekwe Gerezani
Aikaze suruali akimbiye nyumbani
Akimbiye numbani….
Msishikwe na tamaa kama ipo rufani
Hiyo nia ya hadaa Mjitie mitegoni
Halipo na manufaa Ikishapita saini
Ikishapita saini…..