NOIR LA CHAT (PART 1)
Imeandikwa na Abdullah Amur Suleiman
Noir la Chat maana yake kwa Kifaransa ni paka mweusi na kwa desturi zake namna hiyo akikupitia usoni basi usikiuko njia hiyo lakini paka wa Noir la Chat ni wa namna nyengine. Paka wa shirika hilo la biashara ya kibinaadamu hujiuza kwa kustarehesha wanaume, paka wote wakiwa ni wanawake baina ya miaka 18 na 25.
Kwa ilivyokuwa biashara hiyo ni ya aibu/uchafu vile vile naona aibu kuitaja nchi yoyote ambayo shirika hilo lipo. Watu natosoma hekaya hii watakuwa na hamu ya kujua hekaya yenyewe kuliko nchi gani imetokea.
Baada ya kukaa nchi hiyo na kuendelea na kazi zangu baadaye matembezi, mwenyeji wetu ambayo alikuwa akitutembeza tangu mwanzo tulimwona kwamba ni mtu mshonge. Alitutembeza kila mahala na siku moja alituambia kwamba tule chakula chetu cha usiku mapema kwani ametengeza "program" nzuri kwa usiku huo. Sisi ilivyokuwa ni wageni, hatukuweza kumwuliza mwenyeji wetu wapi tutatembelea usiku huo ni jambo hilo si adabu. Mwenyeji akitaka kukutembeza au kukutia mjini basi wewe wajibu wako kukubali kwenda huko na huku ama kwa vitendo hivyo hutegemea nafasi yake kuvifanya au kuvikataa.
Tulipokwisha kula na kunywa vivywaji vya kutia moto na hari, tulishuka nje ya nyumba tuliyokuwa tukikaa na hapo tulikuta motokari tayari inatungojea. Tuliingia ndani ya motokaa hiyo na tukashika njia ya kwenda matembezini. Mimi na wenzangu wawili ndiyo tuliyokuwa ni wageni na mwenyeji wetu mmoja. Shamla yetu ilikuwa ni ya watu wanne tu. Motokaa ilikwenda kiasi ya masafa ya maili tatu na baadaye ilianza kwenda njia za vichochoroni ambao ilitubidi kila hatua chache gari yetu isimame na iende mwendo mdogo mdogo. Mwishowe tulifika pahala tulipokuwa tunakwenda kutembezwa.
Mwenyeji wetu alishuka na kumlipa dereva na kumwambia aende zake na arejee saa sita za usiku na aje kutuchukua. Wakati huo tulipowasili hapo pahala ilikuwa ni saa mbili unsusu usiku. Mwenyeji wetu alipiga hodi na badala ya kufunguliwa kidirisha kidogo kiasi ya kuconekana uso tu kiliochopoka hapo mlangoni na mwenyeji wetu alisema na yule mtu aliyekuwa akichungulia na baada ya maneno kidogo basi mlango ulifunguliwa. Alitangulia yeye kuingia ndani na sisi baadaye tulifuatia nyuma yake. Mara tu ukiingia ndani, kulia kwake kuna "bar" ya kuuziya pombe na vinywaji nyengine vya kuburudika. Kwa upande wa kushoto kulikuwa na wanaume watupu waliokuwa ambao wote walikuwa wamevalia miwani ya jua! Wakati wa usiku na kila mmoja na miwani ya jua. Watu wote hao walikuwa kimya hapana aliyekuwa akizungumza wala sifikiri yupo aliyekuwa akimjua mwenziwe kwani hiyo taa neynyewe ailikuwa haina mwangaza sana. Sisi tu ndiyo waliweza kutujua lakini hata yule mwenyeji wetu hakuweza kuwajua kwamba watu hao ni nani na nani.
Sisi tulikuwa hatuna miwani lakini mwenyeji wetu alipomwita msichana ambaye alikuwa akitumikia hapo kwenye vinywaji na alikuja. Nilipotupa macho kumwona, niliwaza kushughulika kwani siyo ujaji wa desturi. Alikuwa amevaa chupi nyembamba, kifuani, sidiria nyepesi, sehemu zengine zilikuwa wazi. Huu ni mankari. Bila ya kuona haya wala kunena chochote alikuwa hata kwenye meza yetu na baada ya kuchekezana na mwenyeji wetu aliandika orodha ya vinywaji ambavyo tulivihitajia. Tuliweza kunywa namna kwa namna ya vinywaji tangu vile vikali kama kenyak, brandy na wisky. Yule msichana alizidi kuruhahika kwani ilikuwa kama ule usemi wa Kiswahili "mzungu akilewa mkono mfukoni". Mikono ilitiwa mifukoni kwa ajili ya kutoa fedha hata mwishowe ilikuwa tena patupu.
Ulevi maisha ni mbwa na ujibwa wake mara tu ulidhiihiri mara tu alipoanza kupanda kichwani. Wenye vichwa vidogo vyepesi mara waliwaza kwimba na kucheza dansa na yule msichana. Alionesha alikuwa tayari kwa machezo yoyote, vijana waliendelea. Lakini yule mwenyeji wetu alituambia tumalize na twende mahala kwengine katika nyumba hiyo ili tukaone vya miko. Tulimaliza vinywaji vyetu, kulipa fedha na baadaye tuliondoka na kumpa bakhahishi nzuri yule msichana mrembo anbaye tulikunywa vinywaji nyetu akiwa yeye pia ni sehemu ya hayo tuliyokuwa tukimimina tumboni. Tulimuaga na kwenda kwenye ngazi ya nyumba hiyo.
Tulipanda ghorofa ya mwanzo na hapo tulikuta safu za wanaume zimeandamana, mmoja baada ya mmoja kama wananunua stempu posta kwa zama. Ukutani kulikuwa na picha kubwa iliyochorwa juu ya huo ukuta. Picha hiyo ikukuwa ya mwanamke aliyekukwa amelala, hali yake alikuwa ya uchi na paka amesimama mbele yake. Paka huyo alikuwa ni mweusi alini alionesha uaminifu kwani alikuwa hali hicho kitoweo. Jina la pahala hapo pamechukua umaarufu wa picha hii. Picha hiyo imepigwa kwa ufundi na hata hapana mtu yeyeote endayo nyumba hiyo bila ya kuisifu kwa utovu wake wa adabu. Lakini azimiyo la picha hii hasa ni kujaribu kumahawishi yule aendayo Noir la Chat aingiwe na raghba ya kucheza msegesa. Ule usemi na Kiswahili "Ukienda nchi yenye chongo watupu basi toa lake jicho" Yote hatukuyasaza bali tuliyatofoa yote.
Ilikuwa mtindi haukunichukua vizuri hata kunifanya niwe na raghba ya kula vya miko. Mimi si mwepesi wa kuhadaika wala kukubali kula vya miko namna hiyo hasa vile ilivyokuwa mambo yote ni ya kibiashara kuliko starehe. Mtu baada ya mtu walikuwa wakienda vyumba mbalimbali na wakitoka nje huwa "paisa potea" wanafunga suruwali. "Paisa potea" nilijikuta mwenyewe ninasema hivyo. Mambo ni kama hayo shamla shamla tu, mwenye fedha basi apite ndani asiyokuwa nazo basi aje. Nilikuwa nazo pesa lakini nilikuwa nikiona taabu namna ya jambo lenyewe lilivyo. Wasomaji atanisamehe nikiweza kwamba nilikuwa nikiona kama mtu mwenye kutema mate ndani ya tasa lakini tasa lenyewe lilivyokuwa ni chafu hata nikiona uchafu kutena mate yangu humo tasani. Lakini mate yangu ni machafu lakini nilikuwa siwezi kuyatema mate.
Mwenyeji wangu alinitaka na mimi niingiye uchawini lakini niliomba msamaha kwa kusema kwamba hali ya mambo, kwangu ni baridi peop wa mama alinikumba. Alinikubalia na huku akichekekacheka kwa kutumaini kwamba huenda nikamkualia. Waliokwenda, walikwenda lakini ila mimi tu ilikuwa "mmhh simo". Watu huenda kustarehe siri na faragha leo hii binaadamu wamekuwa wakifanya kama wanyama wanaongoja kupandishwa – mambo hayana raha kwa namna hii. Kwa hiyo badala ya kujichoma ndani kama wengine, kazi yangu ilikuwa ni kuhesabu watu wangapi wameingia chumba kimoja. Niliweza kuhesabu kiasi ya nne unusu za usiku hata saa sita za usiku, bibi au kijakazi mmojawapo wa shirika hilo la Noir la Chat alipata wageni kiasi 30! Wete hao walimwelezea yeye na alionesha kwamba bado anaweza kazi zaidi – hakuchoka.
Wakati ulipokwisha nilimwomba yule mgeni wangu anijulishe na yule bibi mvunja rekodi. Mwenyeji wangu alikubali na nilijulishwa nayo na hapo nilmwalika aje kula chakula cha mchana na mimi siku ya pili. Alikataa kwa vile hawezi kufanya kitu chochote ila kwa ruhusa ya "patrons" masomo wa shirika hilo ambalo wao ndiyo wanaliendesha. Wao wakiwa watu au wanawake waliokulia humo humo na kupitisha ujana wao katika biashara hiyo ya uchafu, sasa walikuwa ni wakubwa na nyumba hiyo na kazi yao ni kukusanya fedha, kukutaana wanawake vijana, nyumba na mambo mengineyo yanahusu shirika hilo. Vile vile kwa ajili ya kuendesha shirika hilo iliwabidi watoe sehemu ya pato lao Fulani kuwa ni ushuru wa serikali. Hesabu zote zikiwekwa kwa uangalifu. Yule msichana alipewa ruhusa na "patron" na aliahidi kuja kula chakula cha mchana na mimi.
Hapa nakuona wewe msomaji ukisema, huyu mwandishi anatuzuga, hivyo kweli alikwenda kwenye nyumba hiyo ya uchawi na asiwange. Amekwendea nini basi? Hizo ni fikira zake mwenyewe. Siwezi kukuziya usifikiri hivyo lakini mimi wenyewe siku hiyo sikwangu kwani niliona uwangaji wenyewe si wa kunipendeza wala si wa mikato yangu, kwa hivyo niliupuuza. Nilijulishwa na kiongozi "patrons" na nyumba hiyo na waliniuliza vipi nimestareheshwa na yule msichana ambayo nimemwalika kula na mimi kesho. "Mimi leo sikuweza kufanya kitu kwani hali yangu si nzuri lakini nimependa sana kuonana na huyo msichana na siku nyengine nitaonja visivyoojwa" nilijibu. Jawabu langu halikumfurahisha "patron" kwani ni mwiko mwanamume kuingia ndani humu asilionje tunda lililoharamishwa. Taabu kujizuia hasa kwa vile vijana jike vidogo vidogo vikiwa vimevalia chupi nyembamba na sidiria, vilikuwa vikijipitisha pitisha huku na huku ili kuongeza masisimawaji wa kuzidisha hamu.
Somo huo bila ya kunitia unyagoni walinieleza uroho wa kazi yao, namna gani wafanye kazi wao huwapata na kutoka nchi gani. "Wengi katika wafanya kazi wetu ni vijana waliotoka nchi za Ulaya na ni kidogo tu ambao ni wenyeji. Hii imekuwa kwamba wenyeji walivyoukwa wanajulikana basi wanaona aibu kutenda jambo hili kwa hivyo basi si wageni tunaifanya kazi hiyo. Wasichana wetu wote nina fahari kukueleza kwamba ni baina ya miaka 18 na 25 umri wao. Hatuweki wanawake waliochoka. Wanunuzi wa biashara yetu wanataka vijana madhubuhi ambao maziwa yao yamesimama alisema patron. Nilikuwa na mengi ambayo nilikuwa nikitaka kuyauliza lakini wakati ulikuwa ni dhiki kwani baada ya saa sita nyumba hiyo huwa lazima wanaume wote watoke na biashara kusita.
Tulitoka nje ya Shirika la Noir la Chat na tulimkuta dereva wetu akitungojea. Yeye alituona sisi mbele na alitukimbilia kule tulikukuwepo na kutuongeza kule kwenye gari yetu. Tuliingia katika motokaa tukitetemeka kwani ilikuwa ni baridi isiyokuwa na mfano. Badala ya kwenda kulala tulimwomba mwenyeji wetu atupeleke hoteli. Nchi za nje maisha ya usiku na ya mchana ni namna moja, kila wakati njia zimejaa watu tele, maduka yawazi na magari yaenda huku na huku. Tulikwenda kwenye hoteli moja ya kienyeji na kwa mara ya kwanza tangu kuja katika nchi hii, tuliweza kula chakula cha kienyeji. Kila siku tulikuwa tukila chakula cha Kizungu, ambacho hakina fahari nasi. Tulishindilia vizuri na tukaendoka hapo ila mmoja kitumbo juu!.
Tulikwenda kulala na mara tu baada ya kuweka ubavu mmoja basi ubavu wa pili kulikuwa asubuhi tayari. Tulisuka kama desturi, baada ya kujisafirisha na kuvalia nguo tulikunywa chai ya asubuhi. Wakati mkubwa tulikuwa nao na kuweza kutembea kwa hivyo basi mwenyeji wetu alikuja kutuchukua tukatembea. Tulikataa kupanda matokaa na tulikubaliana sote kwamba leo tutembee kwa miguu yetu ili tupate kuona ila kitu kwa vizri kuliko kupanda motokaa. Tuliingia madukani na kununua vitu vya anasa na kupita njia za ndani ambamo mlikuwa na maduka ya kienyeji pamoja na viwanda vidogo vidogo vifanyavyo kazi za ustadi na mikono za kienyeji. Tulipendekewa sana na sehemu hii ya matembezi yetu, kwani tuliweza kuona kazi za mikono na vipi wananchi wanajua kuzisanii. Tulitia mikono yetu mifukoni tukanunua sanaa hizo kwa bei ambayo sisi tuliona ni ndogo sana kuliko ile fahari ya sanaa hizo zilivyofanywa.
Tulipita mikahawani na kuona watu wanacheza dama na dhuma. Tulmwomba mwenyeji wetu kama atasema na hao watu wacheze na sisi. Bila ya kukawia aliwaomba wazee na alikubali. Tulikwenda kucheza nao. Mimi na mwenyeji wa huko na tuliwatandika mabao matatu. Mgeni hachomi pweza akanuka, lakini wangu aliweze kunuka ndiyo iliyoniandamiza mimi, iliwaandamia wenzangu.
Mwenye makahawa alifurahi sana kupata heshima hiyo ya wageni kwenda kucheza chuna katika mkahawa wake. Kwa kuonesha mapenzi juu ya wageni, alitukirimu kwa chai ya "astarakhona" ambayo ladha yake ilikuwa kubwa kabisa na "strong" kwa hivyo ilitutoa kijasho. Tuliwagana na wananchi wenzetu ambao waliona makazi yetu nao yalikuwa kama kufumba na kufumbua. Walitaka tuendelee na kucheza lakini tuliwataka samahani kwa kuksema kwamba nchi yao ina mengi ambayo watu kama sisi wapita njia tuna hamu ya kuyaona kwa hivyo basi watusiye radhi. Walikubali zile sababu zetu lakini walikuwa shingo upande.
Mwenyeji wetu alituchukua na kututembeza njia zilizochimba chini ya majumba na kutuonesha vile vile vyumba zilizojengwa chini ya ardhi. Milango yake utafikiri kuwa ni madirisha tu, lakini ikifunguliwa ataona daraja zinachukia chini mpaka kwenye kumbi na vyumba. Alituelezea kwamba nyumba kama hizo pamoja na njia zake ziliwasaidia sana katika ule wakati wa akukdai uhuru wao kwani mkoloni alikula amini kwamba hatoitoka nchi hiyo lakini kwa maaazimio matukufu ya wananchi ya kupata uhuru wao, Mungu aliwasaidia.