MSN Home  |  My MSN  |  Hotmail
Sign in to Windows Live ID Web Search:   
go to MSNGroups 
Groups Home  |  My Groups  |  Language  |  Help  
 
Siti Binti SaadSitiBintiSaad@groups.msn.com 
  
What's New
  Join Now
  Tribute to Siti  
  Life of Siti  
  Siti and her Group  
  Siti's Challenge  
  Lyrics by Siti  
  Kijiti  
  Siti Films  
  Siti Books  
  Taarab  
  Siti's Protègè  
  Other Taarab Stars  
  Current Taarab Stars  
  Message Board  
  Old Zanzibar  
  Dancers 1905  
  TAMWA  
  Abdullah Amur Suleiman  
  Siti Article By Suleiman - Part 1  
  Siti Article By Suleiman - Part 2  
  Culture/Utamaduni  
  Kiswahili  
  Kiswahili - 2  
  Mchezo wa Ng'ombe (Bullfight)  
  Noir La Chat (Paka Shume)  
  Noir La Chat (Paka Shume) 2  
  Pictures  
  Calendar  
  Documents  
  Links  
  Articles  
  
  
  Tools  
 

Noir La Chat (Paka Shume)  - PART 2

Walikufa na hao waliokufa waliamini kuwa ni mashahidi. Walikura hawana kinyoango na mauti katika juhudi ya kuikomboa nchi yao. "Unaona uwanja ule alionesha mwenyeji wetu "Mimi mwenyewe nikiwa mmojawapo katika hao tuliokuwa tukipigana na wakoloni kwa silaha za kienyeji na wao walikuwa na silaha za jkisasa walikuwa siku moja na pahala pamoja watu 10,000. Waliokuwa majuruhi 1,000 na walioumia kidogo kidogo 8,000. Kufa au maafa mengine yote yaliyotufika tuliona ni fahari na ni heshima kubwa kwetu kuteseka namna hiyo katika juhudi ya kujikomboa na utumwa wa kigeni. Tuliwalinda mkoloni na aliihama nchi. "Vive la puople Africana" alimaliza hotuba yake mwenyeji wetu.

Tulitembelea marikiti na kuona matunda na vitu kadha wa kadha vikiuzwa. Bei ya mwisho ukilinganisha na ya kwetu – bei yetu ni rahisi. Vitu vitokavyo nchi za nje bei zake zinauma. Tulitembelea kwenye majengo makuwa na maarufu kwa historia yao. Tulitembelea jumba la makumbusho la Majahidina – wtu waliokufa kwenye jihadi na kupigania uhuru. Humo ndani tuliweza kuona picha za wanaume na wanawake bega kwa bega nakijisalimu kufa au kupona lakini nchi yao iwe huru. Nchi yao imekuwa huru – uhuru wenye thamani isiyolipika hayo ni maisha ya watu yaliyoteketea, na hasara nyengine kubwa zilizosababishwa na mapigano ya uhuru. Sote tulikuwa na huzuni zilizochanganyika na jfuraha. Ilikuwa ni jambo la kusikitisha kuona wageni ambao waliitawala nchi hiyo wanawatia wenyeji hasara kubwa kwa kudai haki zao. Vile vile ilikuwa kwetu ni furaha kwa kuona kwamba juhudi za wenyeji haikukwa za bure.

Tulipotoka katika Jumba hilo la Makumbusho, saa za mchana zilikuwa zimeshaanza kuingia na vile ilivyokuwa nina miadi na yule msichana niliyokutana naye jana usiku kule kwenye Shirika la Noir la Chat, Shirika la uchafu. Tulipanda taksi na kukimbilia nyumba tuliyokuwa tukikaa. Sote wane tulionekana kwamba siku yetu hiyo tunaitumia kwa vizuri sana. Atulifika nyumbani na baada ya kushuka kwenye maotokaa, tuliingia ndani na niliptupa jicho kule kwenye chumba cha kupumzikia kiliyopo chini, nilimwona "madamoselle" amebarizi, mkukuu kabisa. Sikuweza kwenda juu tena kubadilisha nguo hali nilijitoma ndani humo na kujitoa kimasomaso kwa yule binti kwa vile nimechelewa kidogo. "Msamaha bila aibu" alijibu msichana huyo kwa sauti nzuri ya Kiarabu. Alikuwa akisema Kifaransa, Kiingereza, Kiarabu, Kigiriki na Kispania. Lini kupata wakati wa kujua hayo yote katika umri wake wa miaka 20, nilishindwa kujua. Alikuwa ni mdogo, kusoma lugha hizo ni rahisi, lakini akizijua. Nilifuatana na mgeni wangu mpaka kwenye chumba changu na baada ya kubadili nguo, tulitoka na kwenda hoteli ilikuwa karibu na ile nyumba tuliyokuwa tukiketi.

Meza ya pekee kwa watu wawili ilikuwa imeandaliwa pembeni na tulichukuliwa na kwenda kukaribishwa hapo. Msichana alikuwa kavalia rasmi kabisa. Nilimpokea mwavuli wake na baadaye nilimsaidia kuvua lile koti lake la baridi, na kulitundika vizuri. Ahsante zilikuwa zikimiminika kinywani kwa kila jambo la heshima nililomfanyia. Alionesha kuwa na adabu zake kamili katika maisha ya kibinaadamu aliyekuwa nayo hivi sasa, si katika maisha ya ile mali mbovu ambayo ndiyo inampatia maisha yake. Mtumishi wa hotelini alikuwa amesimama na alitoa orodha ya chakula cha siku ile. Orodha hiyo nilimpa huyo msichana kwani ni akina mama ndiye wanajua chakula kizri cha kuwalisha akina baba. Aliwaaza kukchagua sahani mbali mbali za chakula na mwishowe alirejesha orodha hiyo yule mtumishi.

Nilitoa kijiluba changu cha uraibu kikiwa na sigareti na nilimkaribisha, binti huyo alichukua sigireti kwa heshima, aliitia kinywani na mimi nilimwashia na alikumbatia mdono wangu kwa miko yake miwili husemi kama kuna upepo mkali anaogopa kile kibiriti kisisimike. Alipokwisha kuwasha sigireti yake, alinyanyua macho yake na kunitazama. Macho yake yalikuwa ni manene, nyusi zilizochongwa na ndefu. Mimi kabisa mpaka hapo ndugu zangu, nilikuwanikijikaza kisabuni. Nahakikisha mwenzenu nilimuuliza jina lake ni nani na alinijibu "Tausi Andulua" aliongeza kusema "vile vile unaweza kuniita Tausi Cardoze" " Inaonesha kama kwenu ni Spain" nilimuuliza "Baba yangu ni Muhispania na mama yangu ni Mwarabu", Waliondoka huko Spain na walikwenda France ambako walifanya Mastakimu yao. Ukoo wetu si watu matajiri wala banyenya bali ni wafanya kazi. Mimi aina ndugu zangu wengine wane, wawili wanaume na wawili wanawake na mimi ndiye kitindamimba. Jumla yetu ni ndugu watano.

Wakati huo supu ilikuwa imekwisha letwa na tulikuwa tukinywa na kumungunyuwa vipande vya mikate. Supu ilikwisha na sahani nyingine ililetwa pamoja na vyakula vya mikalai na machopochopo.

Tulilipa vyote vilivyokuja na Tausi Andalua alionekana kwamba ni mlaji kuliko mimi lakini juu ya ulaji huo tumbo lake lilikuwa limebabataa na ngonge, halikustuka. Tulimaliza kula na baadaye tulianza kuzungumza. "Sitaki kukuweka sana kwani laba utakuwa na kazi kule Noir la Chat nilisema leo ni siku yangu ya mapumziko alijibu Tausi "Kutwa leo sitakuwa na kazi lakini alianza kazi kuanzia saa mbili za usiku hadi saa sita. Kila wiki hupata saa 12 za mapumziko" alisema Tausi. Kutwa ya leo basi utaweza kutumia namna gani" niliuliza "Nimekuja hapa, nitakwenda madukani na baadaye wakati wa jioni nitatembelea kwenye bustani na magharibi nitakwenda kula na kujitayarisha kabisa kwa kazi pevu" alijibu.

Tulikuwa tukitaka kuzidi kuendelea na mazungumzo yetu lakini pahala kama hapa pa kula, wafanya kazi wakiisha kazi zao basi huenda zao nyumbani na sehemu hii ya nyumba kufungwa na haifunguliwi hadi wakati wengine wa kula. Tuliondoka pahala hapo na kwenda zetu kula nyumbani nilikofikia. Tulikuwepo katika ile sehemu ya chini na tulipokuwa tukiingia ndani tulikutana na wale rafiki zangu wakitoka humo ndani. Tuliamkiana na wakawa kama wananiashiria kwamba leo ni siku yangu basi hawataki kuniingilia. Kiliwataka wakae lakini walisema kwamba hawawezi kukaa hapo, uwanja ulikuwa ni wangu tu na bibi Tausi. Sote wawili tulikaa kwenye sofa moja kubwa na kuanza kuzungumza. "Uliseama kwamba wazee wako wako France pamoja na ndugu zake, vipi wewe katika umri kama huu umeondoka kwenu na kujitia katika kazi kama hii"? niliuliza "Jawabu langu lina sehemu nyingi" alijibu Tausi "kwanza napenda kukwambia kwamba maisha yalikuwa si rahisi kwetu, niliwaza kutamani hichi na hichi kwa vile wenzangu waliokuwa rafiki zangu wakivipata walivyovitaka walivyovitaka na mimi ilikuwa ni shida kumilika vitu kama hivyo".

"Ulijaribu kutafuta kazi hata usipate" niliuliza nilijaribu sana. Viatu vyangu vilisagika nyayo na visigino kwa kwenda huku na huku kutafuta kazi. Wale marafiki zangu nilikuwa nikijua kwamba wengine hawapati vitu hivyo makao lakini walikuwa wakijiuza miili yao na wapate mradi wao wa kuvaa vizuri na kuwa machoni mwa watu kuwa anapendeza. Nilijaribu kujizuia nisiinginye mtegoni lakini mwishowe ilinilazimu niingiye kazini. Jambo hilo ni haramu lakini – hiyo ilikuwa ni bidaa yaani kiingiacho mjini si haramu. Niliyavulia maji nguo na niliyakoga. Niliwanza kuharibika kwani nilifanya tamaa kwa hiyo basi nilikutana na shirika moja ambalo kazi yake linafanya kwa siri lakini kazi yake hasa ni kufundisha wasichana mambo ya uchafu na wakiisha elimika kuwapatia kazi nchi nyenginezo. Hata kazi kama hii sikuipata bure kwani ilinibidi kwa miezi Fulani nimelipa fedha wale walionileta huku. Nafikiri unanielewa kwamba mambo yote hapa hapana mapenzi ila kazi tu". Alimaliza Tausi.

"Huwezi kuona kama unayamaliza maisha yako kwa mapema kwa vile kazi unaifanya lazima baada ya muda mchache ikuvunje? Nilimwuliza "Najua hayo ni ndiyo ninaifanya kwa juhudi ili nikija kuanguka, nitajua pa kangukia wapi. Ninawasaidia wazee wangu kwa fedha na mimi mwenyewe ninajaribu kuweka akiba ili ije inifanye siku za shida alisema Tausi "Utanisamehe nikiuliza suali moja nalo vipi wewe huwezi kustarehe" niliuliza "Mimi sistarehe ila huwa nimefanya kazi. Najua wale wajao Noi la Chat huja kwa kustarehe, lakini sisi wajibu wetu ni kazi, kustarehe utakuwa na mtu mmoja lakini leo watu chungu nzima kila siku starehe hiyo ipo wapi? Aliuliza Tausi "vipi siku moja unaweza mwendewa na watu upatao 30 na usiweze kuumia niliuliza "kila kazi ina siri yake, hiyo ni siri lakini dhahiri yake tunaweza au mimi naweza kuwachukua watu 30 au zaidi kwa kutwa moja" alijibu Tausi.

"Hebu niyakinishe. Kweli hapana mapenzi yoyote yapitayo kabla ya kitendo" niliuliza "Hapana kazi tu". Alijibu Tausi. "Kiasi ya miaka mingapi sasa unafanya kazi hii" niliuliza "Mitatu" alijibu Tausi "Vipi unajiona hali yake" niliuliza "Niangaliye mwenyewe utajitosheleza" alinijibu. "Kwa hakika unaonekana katika hali njema na naona hasara kwamba kwa ajili ya hali ya mambo umechagua kazi kama hiyo" nilisema "sikuchagua kazi kama hii bali hali ya mambo imekuwa kama imenilazimisha kufanya kazi hii. Hapa jengine la kufanya ambalo nililiona lina tija ya haraka kuliko hili" alijibu Tausi. "Hebu niambiye katika miaka hiyo mitatu, umetokea kumpenda yeyote katika matajiri wako" niliuliza "sasa umeuliza suali lenye maana. Mimi kweli hufanya biashara lakini nimesumbuka na kijana mmoja ambaye kila siku hunishawishi niwache maisha haya kwani yeye tayari kunioa na kubakia na mimi mpaka kufa" alinijibu "G" "Tena kwa nini hukubali akaoe"? niliuliza "Mimi nimekwisha kukubali lakini roho yangu naiona inasitasita. Si jambo rahisi kulitekeleza na wewe ndiye mtu wa kwanza kukupa siri hii maana kule Noir la chat wakijua jambo hili basi watanifukuza na kunisafirisha.

"Mimi ningekuwa ni wewe basi mara tu ningejichoma na kuolewa badala ya kuwa nafanya kazi ya uchafu" nilisema "sijapata mtu wa kunipa moyo kama wewe unavyonipa na sasa hivi moyo wangu ni mkubwa na najiona ni shujaa na naweza kutekeleza ahadi niliyompa huyo kijana. Atanioa na nitaishi kama mwanamke mwenye heshima yake. Miasha ya kibiaadamu si ya unyama tena. Siku itakaribia ambayo nitaiaga "Noir la Chat" aliomba kwa Mungu. Mimi nilijibu "Amin" "Kwa nini unasema siku zaidi zipite halafu ndiyo ufanye harusi na huyo mpenzi wako"? niliuliza kuna matengenezo chungu nzima yataka kufanywa kabla siku ya hasuri kwa upande mmoja na kwa upande wa pili kila taahira ikiwa nyingi huenda ikawa hatari, sina mtu wa kunipa hoyo na nachelea hata kuwa ahdai hiyo nikuivunja. Wewe tayari kunisaidia" aliuliza "Kama vipi" niliuliza "Sitaki pesa wala robo pesa kutoka kwako lakini jambo niliitakalo ni lile la kunisaidia nipate karatasi ya uwenyeji wa kuweza kuishi hapa kwani shirika la Noir la Chat wakisikia tu kama ninataka kuolewa basi wataifuta na ile dhamana yao ya mimi kubakia nchini humu wataaiondoa na mimi nitafukuzwa na kuendeshwa ka nazaah" alisema "siahidi lakini nitafanya kama niwezavyo ile wewe na mpenzi wake muweze kuishi raha mustaarehe".

"Mwenyeji wako ni mtu mbaya ana madaraka makubwa nchini humu na yeye anaweza kulitengeneza jambo hili kwa haraka bila ya kupoteza wakati na likawa. Tafadhali mwambiye anisaidiye, sipendi kurudi France. Napenda kubakia humu humu nchini na mpenzi wangu" alidai Tausi "Nitajitahidi kukusaidia, lakini mimi nina shaka moja tu. Wewe kweli utaweza kukaa na mtu mmoja baada kwa siku siku nyingi kuwa mwanamke wa kila mtu"? Niliuliza "sikukwa mwanamke wa kila mtu kama inavyojulikana. Nilikuwa hasa nikifanya kazi. Ajaae kutoka kufanyiwa kazi yake nikimfanyia na asiyekuja ilikuwa basi" alijibu nakucheka cheka.

Baada ya wiki moja tangu siku ile niliyoonana na Tausi Andalaua nilipata taarifa ya harusi kwamba yeye anaolewa. Wakati huo nilikuwa nimekwisha mpatia ule waraka wa kienyeji na si kuwa hana hofu. Mimi nilikuwa nidye ndugu yake wa kupanga basi mimi ndiye niliyekuwa baba, mke na nilishuhudia harusi hiyo. Vijana wawili walioana na kutafuta maisha mapya na kuishi kama watu wengine wenye heshima zao. Makusudio yangu ilikuwa kujua nini ukweli wa mambo ya uchafu yaani wanawake wanafurahi kubakia hivyo au kufanya kwa ajili ya ulimwengu umewazonga. Hekaya hii yenyewe ni jawabu kwangu mwaandishi na wewe unasemaje?.

 

Note -  Habari Imebankiwa hapa kwa ruksa ya mwana wa marehemu Abdullah Amur Suleiman

Notice: Microsoft has no responsibility for the content featured in this group. Click here for more info.
  Try MSN Internet Software for FREE!
    MSN Home  |  My MSN  |  Hotmail  |  Search
Feedback  |  Help  
  ©2005 Microsoft Corporation. All rights reserved.  Legal  Advertise  MSN Privacy